HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA KWENYE MKUTANO WA TATU WA BARAZA KUU LA SABA WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA UKUMBI WA KAMBARAGE HAZINA SQUARE TAREHE 20-21. MEI, 2021 JIJINI DODOMA
1
HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA KWENYE MKUTANO WA TATU WA BARAZA KUU LA SABA WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA UKUMBI WA KAMBARAGE HAZINA SQUARE TAREHE 20-21. MEI, 2021 JIJINI DODOMA
Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani mliopo,
Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Jaji Kiongozi,
Mhe. Jaji Mustapher Siyani, Jaji Mfawidhi Dodoma,
Wahe. Majaji Wafawidhi,
Wahe. Majaji wa Mahakama Kuu mliopo,
Mhe. Mtendaji Mkuu wa Mahakama,
Mhe. Naibu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama,
Mhe. Msajili Mkuu wa Mahakama,
Mhe. Msajili wa Mahakama ya Rufani,
Mhe. Mtendaji wa Mahakama ya Rufani,
Mhe. Msajili wa Mahakama Kuu,
Mhe. Mtendaji wa Mahakama Kuu-Dodoma,
Wah. Naibu Wasajili,
Wakurugenzi na Watendaji wa Mahakama,
Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama,
Katibu wa Baraza,
2
Wajumbe wote wa Baraza kwa nyadhifa,
Wageni waalikwa toka TUGHE Makao Makuu,
Ndugu wageni waalikwa,
Mabibi na Mabwana,
Itifaki imezingatiwa,
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, aliyetujalia uhai, afya njema na kutuwezesha kukutana hapa Dodoma siku ya leo. Aidha, nawashukuru viongozi wote wa mabaraza ya Kanda na Mikoa ya wafanyakazi ambao wengi wao mpo hapa leo, kwa kuweza kufanya vikao vya mabaraza hayo na hatimaye sasa kuleta hoja na mapendekezo yenu katika baraza hili kuu katika mhimili wetu.
Naomba pia nitumie nafasi hii kuipongeza Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania kwa kutekeleza takwa hili la kisheria ambalo chimbuko lake ni tamko la RAIS (Tamko Na 1 la mwaka 1970) na sheria nyingine za kazi zinazohimiza kuwashirikisha wafanyakazi katika kufanya maamuzi mbalimbali kupitia mabaraza ya wafanyakazi. Nawashukuru sana wote waliowezesha baraza hili likafanyika hii leo.
3
Aidha nichukue nafasi hii kuwapongeza watumishi wote wa Mahakama kupitia kwenu wawakilishi wao, kwa kuendelea kufanya kazi katika kipindi kigumu tulichopitia cha tahadhari ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya CORONA, ambao umeikumba Dunia tangu mwishoni mwa mwaka 2019.
Nawapongeza sana kwa kuendeleza shughuli za kimahakama katika kipindi chote cha tahadhari na hivyo kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati. Mtakubaliana nami kwamba, pamoja na njia za tahadhali tulizozichukua, matumizi ya TEHAMA yametusaidia sana katika kuendesha shughuli zetu za kimahakama kwa ufanisi mkubwa. HONGERENI SANA.
Napenda kuchukua fursa hii pia, kusisitiza kwamba, matumizi ya TEHAMA sasa ni endelevu na sitegemei mtumishi yeyote wa Mahakama atarudi nyuma, kuhusu matumizi ya TEHAMA. Ni jukumu letu basi, kila mmoja wetu katika maeneo yetu kuhamasishana, na kuhamasisha kwa nguvu zaidi wadau wetu
4
katika matumizi ya TEHAMA katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kimahakama.
Pongezi kwa Wafanyakazi kwa Kufanikisha Utoaji Haki
Kila mfanyakazi wa Mahakama, ana umuhimu na uzito katika dhima ya utoaji wa huduma za haki. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inapowaahidi watanzania haki ya kupata huduma za haki, kila mwaka mzigo wa kuhakikisha watanzania wanapata huduma hizo zimebebwa na mabega ya wafanyakazi. Tukumbuke kuwa, Mahakama ya Tanzania inaposifiwa kwa kufanya kazi kwa weledi, ufanisi na uwazi; tusisahau mchango mkubwa wa wafanyakazi wa ngazi zote.
Nawapongeza watumishi wote kwa kufanikisha Mpango Mkakati wa Miaka Mitano pamoja na programu ya Maboresho ya Miaka Mitano (The Five-Year Judiciary Strategic Plan 2015/16—2019/20 and Citizen-Centric Judicial Modernisation and Justice Service Delivery Project) ambazo zililenga pia kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 (Tanzania Development Vision 2025).
5
Wote tunafahamu kuwa Taasisi nyingi sana zilijitengenezea mipango mikakati. Hata hivyo, Taasisi nyingi hazikutekeleza mipango yake na ilibaki katika makaratasi. Lakini, wafanyakazi wa Mahakama walitekeleza Mpango Mkakati na Programu ya Maboresho, na leo hii mafanikio ya utekelezaji kwa mafanikio unaozungumzwa dunia nzima kama mfano wa kuigwa. Naamini, kujitolea na kujituma kulivyoonyeshwa na wafanyakazi, kutafanikisha utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama mpya wa mwaka 2020/21-2024/25.
Kupitia Baraza hili la Wafanya Kazi, ninawaomba watumishi wote wa Mahakama wajenge tabia ya kufuatilia na kufahamu mambo yote yanayofanyika sio tu ndani ya Mhimili wa Mahakama, bali pia Tanzania na Dunia kwa ujumla. Nawasihi wafanyakazi wote, tujijengee tabia ya kusoma nyaraka muhimu za Mahakama zinazoonyesha Mahakama inatoka wapi na inakwenda wapi.
Tusisubiri kuelezwa yaliyomo ndani ya nyaraka hizi muhimu ambazo nyingi ni nyaraka za wazi na zinapatikana kwa urahisi
6
katika Tovuti ya Mahakama. Lazima mfahamu kinachoendelea pia ndani ya Tanzania.
Mfano mzuri ni wa jambo la kitaifa ambalo linawagusa wafanyakazi wote Tanzania ni suala la uboreshaji maslahi ya wafanyakazi na kupandisha mishahara yao, suala ambalo Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizungumzia kitaifa huko Mwanza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani, tarehe 1 Mei, 2021. Alisema:
“Kauli mbiu yenu mwaka huu, ambayo inasema ‘Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi Iendelee’. Kauli mbiu hii inatoa ujumbe kwa Serikali kuhusu umuhimu wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kupandisha mishahara yao, ambayo natambua kuwa haijapandishwa kwa muda mrefu (takriban miaka 6 kwa sekta ya umma na miaka 8 sekta binafsi).”
7
Aliyoyasema Mkuu wa Nchi kuhusu suala la mishahara, linagusa pia wafanyakazi wa Mahakama, ambao ni sehemu ya wafanyakazi wa Tanzania:
“Naomba sasa nizungumzie suala lililokuwa linasubiriwa kwa hamu kuhusu Mishahara. … kama nilivyosema awali, dai la kuongezewa mshahara ni la msingi na ni kweli mishahara haijaongezwa kwa muda mrefu. Binafsi natamani sana kuona kuwa, mwaka huu, mishahara ya watumishi inaongezwa. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali, nimeshindwa kutimiza matamanio yangu.
…. Hivyo, kwa kuzingatia hayo yote, imekuwa vigumu kwetu kuongeza mishahara kwenye mwaka huu; na hasa kutokana na ukweli kuwa nimeingia madarakani hivi karibuni….
… Lakini, pamoja na ukweli huo; kwa kutambua umuhimu wa wafanyakazi, tunakusudia kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwenye Mwaka ujao wa Fedha.”
8
Ufafanuzi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatuhusu pia, sisi wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania.
MAPINDUZI YA NNE YA VIWANDA (FOURTH INDUSTRIAL REVOLUTION
Katika Mkutano huu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania, ipo ajenda kuhusu: “Matumizi ya TEHAMA kwenye kuboresha shughuli za Mahakama.” Hii ni agenda muhimu sana kiasi kuwa hata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito kuwa watu wote duniani (hasa watu masikini) wajumuishwe kwenye maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa sababu huko ndiko shughuli za kiuchumi, kimaendeleo na kijamii zimehamia [Watu wote wajumuishwe kwenye teknolojia: Gazeti la MAJIRA Jumatano 19 Mei 2021].
Ndugu wajumbe wa Baraza, TEHAMA ndio inaendesha uchumi wa dunia na Wafanyakazi wa Mahakama tusiachwe nje ya matumizi ya TEHAMA. Wafanyakazi tujitayarishe kufanya kazi
9
ndani ya Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (Fourth Industrial Revolution) ambayo wafanyakazi hatuwezi kuyaepuka.
Wafanyakazi, tutakuwa katika nafasi ya kuyaelewa haya mapinduzi ya Nne ya Viwanda endapo tutaongeza juhudi za kujitafutia taarifa mbali mbali kutoka katika mitandao na kujisomea ili kujiongeza. Watanzania tulio wengi, baada ya kuhitimu katika fani mbali mbali, huwa hatujisomei mara kwa mara na kujifunza kuhusu mapinduzi makubwa yanayotokea ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania.
Wafanyakazi tutimize LENGO LA NNE katika DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2025, linasisitiza umuhimu wa watanzania kuwa taifa lenye watu wanaojisomea kila siku, wanaojifunza kila siku na wanaotafuta elimu ya ziada wao wenyewe bila ulazima kupitia mafunzo rasmi—“(iv)-kuwepo kwa jamii inayoelimika vyema na inayojifunza.” Kwa sababu wengi wetu hatujisomei kwa hiyo tunakosa habari kuhusu mabadiliko makubwa yanayoletwa na utandawazi (Globalization), Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information Technologies)
10
hivi sasa, Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (Fourth Industrial Revolution).
Viongozi wetu wa Kitaifa, tayari wametoa tahadhari kuwa Tanzania tutambue kuwa kuna Mapinduzi ya Nne ya Viwanda ambayo yatasababisha mabadiliko makubwa sana katika namna binadamu Duniani anavyofanya kazi, anavyoishi, anavyostarehe na hata anavyowasiliana na wengine.
Nchi zilizoendelea tayari zimeona wingu zito la mabadiliko linalonyemelea, na wao tayari wamegundua na kuona kuwa ujuzi uliopo, kazi nyingi na biashara nyingi ambazo wananchi wao walizosomea, kuhitimu na kupata ajira, zinatoweka kwa sababu Dunia kwa sasa inasukumwa na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (4IR). Mapinduzi haya yanahitaji ujuzi mpya, uzoefu mpya, ambao utatumia teknolojia mpya zinazobadili aina za kazi, ajira, uzalishaji na hata aina za huduma zinazotolewa na wafanyakazi.
Wakati wa kufungua rasmi Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Dodoma, tarehe 13 Novemba 2020, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, alitutahadharisha
11
wafanyakazi na wananchi wote tuwe tayari kwa mabadiliko ya Mapinduzi ya Nne ya Viwanda:
“Mheshimiwa Spika;
Dunia hivi sasa ipo kwenye Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (yaani The Fourth Industrial Revoulution) ambayo yanaongozwa na sekta ya mawasiliano (ICT). Shughuli nyingi Duniani, kwa sasa, zinafanyika kwa kutumia TEHAMA. Hivyo basi, sisi nasi hatuna budi kwendana na kasi hiyo ya kukua kwa sekta ya mawasiliano.”
Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan, naye alisisitiza tena yale yaliyosemwa na Rais wa Awamu ya Tano kuhusu hayo mapinduzi ambayo yatagusa namna tutakavoweza kufanya kazi. Alipolihutubia Bunge la 12 jini Dodoma, 22 Aprili, 2021, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, alisema:
12
“Mheshimiwa Spika;
Mbali na miundombinu hiyo migumu, tutaimarisha pia miundombinu laini, hususan miundombinu ya TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO. Kama inavyofahamika, Dunia ipo kwenye Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, ambayo yanaongozwa na sekta ya Teknolojia ya Mawasiliano (TEHAMA), na kwa maana hiyo, Uchumi wa Dunia pamoja na shughuli nyingi duniani, kwa sasa, zinafanyika kwa kutumia TEHAMA. Hivyo basi, sisi Tanzania nasi hatuna budi kuweka mkazo mkubwa katika kukuza sekta hii.”
Sina uhakika kama wafanyakazi wa Mahakama tumesoma Ujumbe wa Mbio za Mwenge kwa Mwaka huu (2021). Ujumbe huo unasema: “TEHAMA NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU, ITUMIE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKAJI.”
Naomba tumsikilize kwa makini sana ndugu Kalage Judas Enock (Mkurugenzi wa TEHAMA) atakapotukumbusha uwekezaji mkubwa ambao Mahakama ya Tanzania imefanya katika
13
TEHAMA ili zituisaidie katika shughuli za kila siku za Mahakama na kuitayarisha Mahakama kuchota faida za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda.
Juhudi hizi na uekezaji mkubwa katika TEHAMA hazitazaa matunda tunayotarajia, endapo wafanyakazi na watumishi wote hawatakuwa sehemu ya mapinduzi ya nne ya viwanda. Naiomba Menejimenti, wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu na Mkurugenzi wa TEHAMA, wawatayarishe watumishi wote kwa mafunzo ya TEHAMA kazini.
Ukisoma nyaraka zetu za maboresho tunazungumzia kuifikisha Mahakama ya Tanzania katika hadhi ya E-JUDICIARY, yaani MAHAKAMA INAYOTOA HUDUMA ZOTE ZA HAKI na zinazowezesha utoaji haki, kufanyika kwa njia ya mtandao. Kila mtumishi lazima awe sehemu ya SAFARI hii ambayo lazima tuwavute wadau wetu muhimu.
Wakati wa kuwakubali Mawakili tarehe 21 Disemba 2020, nilimkaribisha Balozi Mstaafu, Ami Ramadhan Mpungwe, atoe mada kwa Mawakili, kuwatahadharisha kuwa wasipobadili
14
namna wanavyofanya kazi za uwakili, kazi zao zitapotea hivi karibuni na watajikuta wana vyeti vinavyothibitisha kuwa na elimu ya sheria; lakini bila ya kuwa na ajira linganifu na vyeti hivyo.
Tahadhari hiyo inawahusu pia watumishi wote wa Mahakama, kazi na ujuzi tulionao leo utakosa ladha chini wa mabadiliko makubwa ya teknolojia ya Habari na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda. Yapo maandiko yanayosema kuwa, Mapinduzi ya Nne ya Viwanda yaweza kuchukua hadi asilimia 50% ya kazi zinazofanywa sasa hivi na wanasheria, mahakimu na majaji.
Balozi Mpungwe aliwakumbusha Mawakili kuwa maendeleo makubwa yaliyofikiwa katika teknolojia ya Habari, imefungua njia kwa ujio wa Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (4IR), ambayo imeleta mabadiliko katika TAKWIMU KUBWA (big data), uchambuzi wa takwimu (Analytics), akili bandia (Artificial Intelligence), mtandao wa mambo (Internet of Things), kujifunza kwa mashine (machine learning), roboti (Robotics), matumizi ya mahesabu kutatua changamoto (Algorithms), technolojia ya kukusanya taarifa kwa matumizi sehemu mbali mbali kwa hali
15
ya usalama (Block chain technology) na kadhalika. Kwa mujibu wa Balozi Mstaafu Mpungwe, mabadiliko haya, yamebadilisha na wakati mwingine kuvuruga kabisa hali na aina za biashara na shughuli mbali mbali za kitaalamu.
Mabadiliko haya yamebadili na yanaendelea kubadili namna binadamu anavyofanya kazi, anavyoshirikiana na kuwasiliana na binadamu mwenzake na hata kwenye masuala ya starehe na kupumzika. Balozi Mstaafu Mpungwe anasisitiza umahiri wa uongozi (leadership) ndani ya Taasisi kama Mahakama, uongozi; katika biashara na kadhalika ambao utawasaidia watumishi kufanya kazi katika Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, anasema kuhusu umuhimu wa kuwa na uongozi thabiti katika ngazi zote za utumishi:
“This, therefore, requires leadership in different professions and many other areas of human endeavor to start envisioning the future of their respective businesses and professions, in the context of the developments that arise out of the evolving Fourth Industrial Revolution, in order to
16
future proof their professions and their continued relevance.”
Mtaalamu Elekezi wa Mahakama kutoka kampuni ya Estonia, tayari ameshatayarisha barabara ambayo Mhimili wa Mahakama utafuata hadi kufikia E-JUDICIARY (MAHAKAMA MTANDAO). Wafanyakazi ni lazima waelimishwe kuhusu huu mwelekeo ambao utabadili namna wafanyakazi watafanya kazi katika MAHAKAMA MTANDAO (E-JUDICIARY). Tutalazimika kufanya kazi tofauti na tunavyofanya sasa hivi.
Kwa sasa Mahakama ya Tanzania tunatumia TEHAMA kivipande vipande. Safari ya Mahakama ya Tanzania ni kufikia MAHAKAMA MTANDAO (E-JUDICIARY), ambayo ngazi zake zote za utoaji haki, na shughuli zote za kimahakama hutumia TEHAMA na kuachana kabisa na majalada na makaratasi. Wafanyakazi watakaotoa huduma ni wafanyakazi waliopo, ambao watatoa huduma za ki-TEHAMA kama—
• E-Case Management (Mfumo wa Usimamizi wa mashauri kielektroniki);
17
• E- Asset-Management (Mfumo wa usimamizi wa mali kielektroniki);
• E-Document Management (Mfumo wa usimamizi wa nyaraka kielektroniki);
• E-Records Management (Mfumo wa usimamizi na utunzaji wa kumbukumbu kielektroniki);
• E-Human Resource Management (Mfumo wa usimamizi wa rasilimaliwatu kielektroniki);
• E-Complaint Management System (Mfumo wa usimamizi wa malalamiko kielektroniki) ; na
• E-Library Services (Mfumo wa huduma za maktaba kielektroniki).
Nawasihi viongozi, tunayo wajibu na jukumu la kuwatayarisha wafanyakazi na watumishi wote wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi katika mazingira ya MAHAKAMA MTANDAO. Mimi naamini, wajumbe wa Baraza hili, mtafikisha kwa wafanyakazi wote wa Mahakama ujumbe kuhusu mabadiliko makubwa ya Matumizi ya TEHAMA ambayo wafanyakazi wote wanatarajiwa kushiriki kikamilifu.
18
Napenda kuwasisitiza tena kuwa Baraza Kuu hili, ni muhimu sana na ni chachu ya mahusiano mazuri baina ya uongozi na watumishi katika maeneo yetu ya kazi. Aidha kupitia baraza hili ushirikishwaji wa watumishi wote wa Mahakama unafanyika kupitia uwakilishi wenu, hivyo basi mnapata fursa ya kutoa ushauri na kushiriki namna ya kutekeleza majukumu yetu ya Kikatiba ya utoaji wa haki katika Nchi yetu. Hivyo basi mashirikiano yenu katika baraza hili mtambue kuwa ni muhimu sana mustakabali wa dhima ya Taasisi yetu.
Aidha, nimepewa taarifa kuwa katika Baraza hili kutafanyika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa awamu nyingine ya miaka mitano ambayo ni Mpango Mkakati wa Mahakama 2021-2025, kama nilivyogusia hapo awali, sote ni vema tukaufahamu Mpango Mkakati huu na kuusambaza kwa watumishi wenzetu, na hii ni kwa sababu utaratibu huu unalenga kukuza uwazi na ushirikishwaji katika maamuzi mbalimbali ya Mamlaka ili mfanyakazi anapotekeleza majukumu yake awe akifahamu Mpango Mkakati wa Miaka mitano ijayo na unamtaka afanye nini.
19
Ndugu wajumbe na wageni waalikwa, ni matarajio yangu mwisho wa kikao hiki tutatoka na uelewa wa pamoja katika kujua tuko wapi, na malengo yetu ni yapi, maazimio ambayo tutatokanayo katika Baraza hii, nawaahidi hayatabaki kwenye makabati na kwenye mafaili, tunakwenda kuyafanyia kazi na kutimiza matarajio yenu ya kitaasisi.
Kabla sijahitimisha, ninawashukuru sana kwa matayarisho na makaribisho mazuri hapa Dodoma. Kipekee niwashukuru viongozi wa Kanda ya Dodoma Mhe. Jaji Mfawidhi-Dodoma, Naibu Wasajili, Mtendaji wa Mahakama wa Kanda ya Dodoma pamoja na watumishi wote wa Kanda hii. Asante sana kwa kazi nzuri na ukarimu wenu.
Ndugu wajumbe wa Baraza, Napenda kuhitimisha hotuba yangu kwa kuwashukuru tena wafanyakazi wote wa Mahakama pamoja na Viongozi kwa kuiendelea kutimiza majukumu yenu. Niwahakikishie tena mimi kama kiongozi wenu nitaongoza wenzangu wa Makao Makuu kushughulikia yale yote mtakayotushauri na kupendekeza.
20
Ni imani yangu kuwa yote yatakayojadiliwa na kufanyiwa maazimio yatasaidia katika kuboresha kazi yetu ya utoaji haki ya Mahakama ya Tanzania na hivyo kuongeza tija na ufanisi.
Sasa natamka rasmi kuwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania,umefunguliwa rasmi.
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA